MJASIRIAMALI NI NANI?



(sifa za mjasiriamali)
-Ni mtu ambaye yuko tayari kuthubutu.
-Ni mtu ambaye ni mbunifu,
Ni mtu jasiri asiye ogopa kufeli au kushindwa.
-Ni mtu ambaye kilasiku anatafuta njia mpya za kuzalisha na kuleta upya na mabadiriko.
-Ni mtu mvumilivu.
-Ni kiongozi.
-Ni mshindani asiyekata tamaa.
-Ni mtu ambaye anapenda kuwajibika na kazi kwa bidii.
-Ni mtu anayetazama maisha ya mbele.
-Ni mtu ambaye anaweza kubadirisha na kutumia nafasi kama fulsa.
-Ni mtu ambaye anahitaji na anaufahamu dhidi ya mafanikio.
-Ni mtu ambaye anaweza kujitegemea.
Je wewe unasifa hizo hapo juu?
Lakini sio lazima uwe nazo zote zilizo orodheshwa hapo juu, hata sifa chache tu zina kufanya uwe mjasiriamali. kitu cha kuzingatia ni kwamba baadhi ya sifa mtu huzaliwa nazo na zingine mtu hujifunza tu, hivyo nawe unaweza jifunza na ukawa mjasiriamali mkubwa na mwenye mafanikio.
JE UPOTAYARI KUWA MJASIRIAMALI?
kama unata kuwa mjasiriamali basi jibu maswali yafuatayo, kama majibu yako yatakuwa ndio basi wewe ni mjasiriamali lakini kama majibu yako hayatakuwa sio basi unaweza kujipanga upya na ukatafuta namana nyingine ya kueweza kuwa mjasiriamali labda kwa kujifunza dhana za ujasiriamali.
maswali
1. je umejiandaa kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo?
2. je upo tayali kukumbana na kutatua matatizo na changamoto?
3. je unayafahamu vizuri mazingira unayoishi na je upo tayali kuyatumia na kuanzisha jambo jipya?
4. je upotayari kusubili kwa muda mrefu matunda ya juhudi zako?
FAIDA ZA UJASIRIAMALI
kukuza na kuendeleza uchumi katika nchi
kupunguza umasikini miongoni mwa watu
ujasiriamali hutusaidia kutumia ipasavyo rasilimali tulizonazo
matumizi sahihi ya rasilimali watu
ujasiamali hutupa mwanga katika kufanya na kuanzisha shughuri mpya
ujira binasfsi na nafasi za ajira kwa watu wengi
hupunguza kiwango cha umasikini miongoni mwa watu
hupunguza tofauti katika maendeleo baina ya watu, mikoa, nchi n.k
VITU VINAVYOMJENGA MJASILIAMALI
MTAJI
FURSA
UBUNIFU
MAWASILIANO
MTAJI
ni kitu chochote ambacho mjasiliamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo flani kwa lengo la kupata faida. mtaji umegawanyika katika miundo ifuatayo:- mtaji wa fedha,nguvu kazi,mtaji jamii,elimu na utaalamu katika jambo flani.
FURSA
Fulsa ni kama uti wa mgongo kwa mjasiliamali. mjasiliamali lazima awe na uwezo wa kutambua au kugundua fulsa, uwezo wa kuchambua na kuchanganua fulsa pia kuchukua hatua juu ya fulsa husika.
UBUNIFU
Kwa kawaida mjasiliamali anatakiwa kuwa mbunifu, ubunifu ndio unamtofautisha mtu mmoja na mwingine hata kama wote watafanya jambo linalo fanana. kilasiku unatakiwa kufikili ni jinsi gani utafanya jambo jipya ua jambo lililofanya na wengine lakini wewe ufanye katika njia tofauti.
MAWASILIANO
Mawasiliano huunganisha vitu pamoja na huweka watu pamoja na husaidia kupata taarifu huhimu katika biashara yako.
Mawasiliana huunganisha mtaji, fulsa na ubunifu, mjasiliamali anatakiwa kuboresha mawasiliano ili afanikiwe katika ujasiliamali wake.

Tafadhali tuandikie maoni yako hapo chini!

Washirikishe wengine makala hii.

Comments

    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment